KWA NINI NILIAMUA KUACHANA NA UISLAMU NA KUWA MKRISTO?” Sehemu ya 13

Na Mtumishi wa MUNGU, Abel Suleiman Shiriwa.
Ushuhuda wa ajabu sana unaendelea, na kama kukusoma sehemu zilizotangulia basi Sehemu ya kwanza FUNGUA HAPA Na Sehemu ya pili FUNGUA HAPA Na kwa sehemu ya tatu FUNGUA HAPA.
Kwa sehemu ya 4 FUNGUA HAPA
Na kwa sehemu ya 5 FUNGUA HAPA na sehemu ya 7 ni FUNGUA HAPA
Nikamuona HAJI SALUM anainua ule mkono ulioshika jiwe, Nami nikamkazia macho kumwangalia, nimuone atafanya nini, kwani yeye alikuwa ananifahamu kuwa nilikuwa mkorofi, tulipokuwa Madrasa nilikuwa naogopeka kwa sababu ya ukorofi alipoona sitishiki, akalitupa jiwe, wakati huo huo Wakristo, wakaja pale tulipokuwepo, na kuanza kuwatoa wale Waislamu pale. HAJI Wakati anaondoka, akawa anasema, “LAANA TULLAH ALAYKA” (Laana ya Allah iwe juu yako) Mimi wala hata sikujali, kwani nilijua laana yake ni sawa na mtu kujilisha Upepo,
Mithali 26:2 Kama shomoro katika kutanga-tanga kwake, Na kama mbayuwayu katika kuruka kwake; Kadhalika laana isiyo na sababu haimpigi mtu.
Kwa hivyo sikutishika chohote na laana ile, ila nikawa nawaza tu kuhusu nauli ya mama ambayo nimepewa kwa ajili ya kwenda huko kutangaza Da”awa ya kiislamu, nikajipa moyo kuwa, liwalo basi na liwe, Hassan, akanifuata na kuniuliza, “Vipi huyo jamaa uliekuwa unaongea nae, mnafahamiana?” Nikawambia ‘Ndiyo, nimesoma nae Thaqaafa, akasema, “Tunamshukuru Mungu kwa kuwa hakuweza kukudhuru” Mkutano ule ukaendelea kama kawaida baada ya kuondoshwa pale wale waislamu,, kwa kweli kuishi kule Ukerewe kulinifanya niweze kuimarika katika Imani kupitia mafundisho ya Kikrsito ambayo niliyapata kutoka Kanisa lile la E.AG.T ambalo msimamizi wake, ni Mchungaji Michael Abel, Mkutano ule ulikuwa ni wa siku 30
Kadiri ambavyo niliendelea kukaa kwenye mkutano ule ndivyo nilivyozidi kuimarika katika imani, baada ya zoezi lile la Wale Vijana wa MARKAZ ALJAZEERA, Kushindwa kufanikiwa zoezi lao, la kufanya fujo, ikabidi, wawaite wahadhiri kutoka Mwanza, kina Issa Kalenga, IDD Pengo, na wengineo, Kweli wakaja pale Ukerewe, lakini kwenye meza yetu hawakuwa wanakuja, bali walikuwa wakimtuma jamaa mmoja hivi anaitwa Omary, (BONDIA) aje pale kuuliza, lakini nae hakuweza kufua dafu, wakaamua nao kuanzisha muhadhara wao msikitini, ili kuwazuia Waislamu wasije kwenye mkutano wetu, lakini hawakuweza kufanikiwa, kwani waislamu wakawa wanakuja kutusikiliza, wakati wote huo wa mkutano, mimi na Hassan, hatukuwa tukipeleka somo lolote, (Ila mimi nikawa nasoma aya za quran kwa kiarabu) kwani tulitakiwa kwanza tujifunze kwanza Kuhusu Imani ya Kikrsto, ili tukishaifahamu, basi tuweze kuishindania vema imani, kama maandiko yasemavyo.
Yuda 1:3 Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu.
Ule Mkutano ukawavuta watu wengi sana, na ukizingatia kachumbari yangu ya Kiarabu ikawa inawafanya watu wengi wahudhurie kwenye mkutano ule, Kina Issa Kalenga walipoona kule wamekosa watu, ikawabidi waje kule kwetu, Siku hiyo, Uwanja ulijaa kweli, likapelekwa somo la Yesu siyo Issa, Issa Kalenga akawa amekaa pale mezani, baada ya muda wa somo kuisha, akakakribishwa kuuliza, swali lake, basi akaomba asomewe Quran, 3:45
إِذْ قَالَتِ الْمَلَآئِكَةُ يَا مَرْيَمُ إِنَّ اللّهَ يُبَشِّرُكِ بِكَلِمَةٍ مِّنْهُ اسْمُهُ الْمَسِيحُ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ وَجِيهًا فِي الدُّنْيَا وَالآخِرَةِ وَمِنَ الْمُقَرَّبِينَ
45. (Kumbukeni) Malaika waliposema: Ewe Mariam! Hakika Mwenyeezi Mungu anakupa khabari njema za neno litokalo kwake, jina lake ni Masihi Isa Mwana wa Mariam, mwenye heshima ulimwenguni na Akhera, na ni miongoni mwa wenye kukurubishwa (mbele ya Mwenyeezi Mungu).

Akasema, “Kwa mujibu wa andiko hili, tunaambiwa kuwa, Mama yake na Issa, hapa anaitwa Mariamu, nanyi mmesema Yesu na Issa ni wawili tofauti, ili ionekane kuwa hawa ni wawili toafuti, Je kwa Mujibu wa BIBLIA mama yake na Yesu, Jina lake anaitwa nani?”
Alivyouliza vile, nikawa namtamani kweli nimkaange, Nikawambia ERNEST, “Nipe mimi nimjibu hilo swali” Akasema, “Swali lako tumelisikia, sasa mimi sitokujibu, nitakukabidhi mwanafunzi wangu, ambae alikuwa huko kwenye imani ambayo upo wewe, nae pia kabla ya kuja kwa Yesu, alikuwa anauliza maswali kama hayo, sasa, leo nataka niwakutanishe na mwanafunzi wako wa zamani, ambae kwa sasa ni mwanafunzi wangu, Karibu Aboubakari” Basi nikainuka pale na kushika microphone, Nikasema,
“Namshukuru sana Sana Bwana Yesu Kristo kwa nafasi hii ambayo amenipa, kwani leo nimepata nafasi ya kusimama na kuweza kumpa darasa aliyekuwa Mwalimu wangu wa Madrasa, Issa Kalenga, pale THAAQIBU, kabla ajaachakufundisha na kujiingiza kwenye Mihadhara, Makofi yakasikika, ametoa andiko eti mama yake na Issa, ameitwa Mariamu, kwa kuwa ameitwa Mariamu, akataka kujua kwa mujibu wa Biblia,mama yake na Yesu anaitwa nani ili waonekane kuwa ni wawili tofauti? Yaani kwa akili yake akiwa ni Mariamu basi ndo huyo, JIBU langu ni kwamba, mama yake na Yesu, anaitwa Mariamu” Nilipojibu anaitwa Mariamu, waislamu wakapiga Takbiriiiiiii, kuonesha kuwa eti wameshinda, basi mimi nikacheka, nikasema Hizo Takbiira zenu baadae pia muendelee kuzipiga, nikamwambia msomaji mpe Kalenga Mic, akapewa, Nikamwambia,
“Kwa mujibu wa BIBLIA, Mama yake na Yesu, anaitwa Mariamu, umenielewa?” akawageukia waislamu, Akasema, “Waislamu Takbiir” Wakaitikia “Allahu Akbar”, akarudi kwangu, na kusema, ‘Umejibu vema, kama ni Mariamu, inakuwaje sasa mseme ni wawili tofauti?” Nikamwambia, “Naam hapo sasa ndo umeuliza swali la msingi sana, lile la Mwanzo ulikurupuka, na waislamu wenzio bila kujua wakakupigia Takbiir, wakidhani kwamba, umewakomboa, na kumbe ndo umewaangusha, kwa sababu kama Yesu ni Issa, basi na wewe jina lako unaitwa Isaa, unataka kutuambia nawe ni Yesu? sasa kwa kuwa hoja yako umeijengea kwenye Mariamu, basi me nakupa andiko kuhusu Mariamu, halafu nitakuuliza swali, ukiweza kulijibu ipasavyo hapo ndo utajua ni kwa nini tunasema kuwa Issa na Yesu ni wawili tofauti” Nikamwambia mjuni, hebu nisomee
Yohana 19:25 Na penye msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mamaye, na umbu la mamaye, Mariamu wa Klopa, na Mariamu Magdalene
Nikamwambia Mjuni, “Mpatie mic Kalenga” Akampa Mic, Nikawambia, wewe hoja yako ipo kwa Mariamu, kwa kuwa mama yake na Issa ameitwa Mariamu, na mama yake Yesu, nae ameitwa Mariamu kwa hivyo ni mmoja, Kwa mujibu wa andiko halo hapo, Limewataja Mariamu wangapi?”
Akajibu kwa kusema, “Mariamu watatu” nikamuuliza, “Ni Mariamu yupi na yupi?” Akasema, “Mariamu mama yake na Yesu, na Mariamu Waclopa, na Mariamu Magdalene”, Nikamuuliza, “Je! Hao wote watatu wamemzaa Yesu?” Akasema, ‘Hapana? (Makofi kwa Wakrito yakasikika) Hapo Takbiira za Waislamu zikanywea, hawakusikika tena wakipiga Takbira, Basi Nikamwambia Issa Kalenga, kuwa, hoja ya Mariamu kwa kutaja jina siyo tatizo, hapa hoja ya msingi ni kuwa Je namna ya kuzaa kwao huyo mama yake na Issa na mama yake Yesu ni sawa? Ukishajua hivyo basi unapata jibu, maana mwenyewe hapo umewaona Mariamu watatu, kuna Mariamu mama yake Yesu, na kuna Mariamu Waclopa, na Mariamu Magdalene, na katika Mariamu hao watatu ni mmoja tu ndiye alimzaa Yesu, sasa ngoja nikufundishe tofauti iliopo kati yan mama yake Issa na Yesu.
Kwanza kabisa, nikairudia ile aya yake ambayo alikuwa ameitoa Quran 3:45
Nikawambia kuwa, hapo kwa mujibu wa andiko hilo, Imesemwa kuwa, Malaika waliposema,….. Hivi waliposema, ni umoja au wingi?” Akajibu kuwa, ni “Uwingi”
Nikawambia, naam, sasa naomba utulie nikupe darasa, nikamwambia msomaji aome tena Quran 19:16 Surat Mariam

وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ مَرْيَمَ إِذِ انتَبَذَتْ مِنْ أَهْلِهَا مَكَانًا شَرْقِيًّا
16. Na mtaje Maryam Kitabuni alipojitenga na jamaa zake, (akaenda) mahala upande wa mashariki (wa msikiti)
. na akaweka pazia kujikinga nao, kisha tukampelekea muhuisha sheria yetu (Jibril) aliyejimithilisha kwake (sura ya) binadamu alie kamili.
18. (Maryam) akasema: Hakika mimi najikinga kwa Mwingi wa rehema aniepushe nawe, ikiwa unamuogopa (Mwenyeezi Mungu ondoka zako).
19. (Malaika) akasema: Hakika mimi ni mjumbe wa Mola wako, ili nikupe mwana mtakatifu,

Nikamuuliza, hapo kumetajwa Malaka wangapi? Akajibu, “Mmoja” na kule kwenye Quran 3:45 kumetajwa malaika wangapi? akajibu, “Wawili” Nikamwambia huoni kama huo ni mkanganyiko? Iweje kule wawe wengi, halafu huku mmoja? Na isitoshe Tunaambiwa, kuwa, Mariamu aliijtenga na jamaa zake, akaenda mashariki mwa msikiti, tena akawa ameweka pazia ili kujikinga na jamaa zake wasimuone, (Hapo ni lazima alikuwa na miadi na mtu, ya kukutana nyuma ya pazia ndiyo maana akaweka pazia) Kisha akapelekewa, Jibril ambae yeye akaingia kwa umbile la Mwanume alie kamilika, (Hii ya Mwanume alie kamili, inajulikana wazi kuwa, siyo Khanisi, ni mtu mwenye uwezo wa kufanya tendo la ndoa, Mariamu mamake Issa, alipoona sura ya mwanaume mgeni, basi akaogopa, akaamua kumfukuza, Kwa nini alimfukuza? Ni kwa sababu alipoweka pazia, hakuwa na miadi ya kuonana na Jibiril, bali mtu mwingine, Jibril akajitambulisha kuwa yeye ni mjumbe wa Mola wa Mariamu, Ili Jibril ampe Mariamu mtoto, (Hapa inaonesha kuwa Issa ni mtoto wa Jibril) maana kasema, ili nikupe mwana, sijui alikuwa amemuweka kwenye mfuko wa Suruali, Ndiyo maana Waislamu hukataa kusema Issa ni Mwana wa Mungu, kwa sababu wanajua ni mtoto wa Jibril, wakati Biblia imesema Yesu ni mtoto wa Mungu.
Sasa ona tofauti ya ya habari za kuzaliwa kwao, Mwangalie Yesu hapa.
Luka 1: 26 Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti,
27 kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu.
28 Akaingia nyumbani kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe.

****Hapa tunaona Malaika alipoingia nyumbani kwa Mariamu, wakati yule mama yake Isa yeye alikuwa upande wa mashariki wa msikiti, Gabriel hapa, akamsalimu Mariamu kumtoa khofu, wakati kwenye Quran, Jibril hakusalimia, tena aliingia kwa umbo la mwanaume alie Kamili, Wakati Gabriel yeye ameenda kwa umbile la Kimalaika na kumsalimu Mariamu, kuwa amepata Neema kwa BWANA****
29 Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani?
30 Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu.
31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.

**Hapo Mariamu akastuka kusikia habari hizo, lakini malaika akamwambia, kuwa, Usiogope, wakati kule kwa Jibril, hakuambiwa usiogope, bali alichoambiwa ni kuwa, mimi ni mjumbe wa mola wako ili nikupe Mwana**
32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.
33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho.
34 Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume?
35 Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.

Gabriel akasema kuwa, Yesu atazaliwa kwa uwezo wa ROHO MTAKATIFU, tena Mariamu akaambiwa kuwa utachukua mimba, “Hicho ni kipindi kichacho” tena ataitwa Mwana wa alie juu, Wakati mama yake Issa yeye baada ya mazungumzo na Jibril akachukua mimba pale pale
Quran 19:
قَالَتْ أَنَّى يَكُونُ لِي غُلَامٌ وَلَمْ يَمْسَسْنِي بَشَرٌ وَلَمْ أَكُ بَغِيًّا
20. Akasema: Ninawezaje kupata mtoto hali hajanigusa mwanamume yeyote wala mimi si asherati.
قَالَ كَذَلِكِ قَالَ رَبُّكِ هُوَ عَلَيَّ هَيِّنٌ وَلِنَجْعَلَهُ آيَةً لِلنَّاسِ وَرَحْمَةً مِّنَّا وَكَانَ أَمْرًا مَّقْضِيًّا
21. (Malaika) akasema: Ni kama hivyo, Mola wako amesema; Haya ni rahisi kwangu, Na ili tumfanye Muujiza kwa watu na rehema itokayo kwetu, na ni jambo limekwisha hukumiwa.
فَحَمَلَتْهُ فَانتَبَذَتْ بِهِ مَكَانًا قَصِيًّا
22. Basi akachukua mimba yake, na akaondoka naye mpaka mahala pa mbali.
فَأَجَاءهَا الْمَخَاضُ إِلَى جِذْعِ النَّخْلَةِ قَالَتْ يَا لَيْتَنِي مِتُّ قَبْلَ هَذَا وَكُنتُ نَسْيًا مَّنسِيًّا
23. Kisha uchungu ukampeleka penye shina la mtende, akasema: Laiti ningekufa kabla ya haya, na ningekuwa niliyesahaulika kabisa.
فَنَادَاهَا مِن تَحْتِهَا أَلَّا تَحْزَنِي قَدْ جَعَلَ رَبُّكِ تَحْتَكِ سَرِيًّا
24. Mara ikamfikia sauti kutoka chini yake: Usihuzunike, hakika Mola wako ameweka kijito chini
25. Na litikise kwako shina la mtende, litakuangushia tende nzuri, zilizoiva.
sitasema na mtu.

27. Kisha akampeleka kwa jamaa zake akimbeba. Wakasema: Ewe Maryam! hakika umeleta kitu cha ajabu.
28. Ewe dada ya Harun! baba yako hakuwa mtu mbaya wala mama yako hakuwa asherati.
29. Ndipo akaashiria kwake, wakasema: Tuzungumzeje na mdogo yumo katika mlezi?

Baada ya mazungumzo Mama yake na Issa akachukua mimba akaondoka nayo siku hiyo hiyo, na akajifungua siku hiyo, wakati anajifungua, Ndipo Sauti kutoka kwa Mola wake ikasikika kutoka chini, yaani sauti ikasikika sauti ya mola wa Issa, wa Issa ikimtaka atikise shina la mtende, (yaani hapo mwanamke anajifungua anaambiwa atikise shina la mtende) Mtende ugumu wake ni kama mnazi, mimi sijui kama mwanamke anaejifungua, anaweza hata kuomba simu ambipu muwewe, seuze kutikisa shina la mtende? na kwa mujibu wa BIBLIA huko chini, (Ambako imetokea sauti ya mola wa Issa) ni kuzimu,
Mithali 15:24 Kwa mtu mwenye akili njia ya uhai huenda juu; Ili atoke katika kuzimu chini.
Na Isitoshe, Shetani alitupwa Chini
Ufunuo 12: 9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
Sasa kama ikiwa Mola wa Issa sauti yake inatoka Chini, huoni kwamba huyu Isa yeye ni wa shetani? Sisi kwa Yesu Yesu wetu Sauti haitoki chini, bali juu
Mahayo 3:16 Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake;
17 na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.

Kwa hivyo nikawambia Kalenga kuwa, Issa hawezi kuwa Yesu, kwa kigezo cha Mariamu, kwani japokuwa habari zao zimefananishwa, lakini habari za Issa zina makosa makubwa sana, kwani ni habari mbili tofauti, kwani Quran 3:45 Ilisema kuwa Mariamu mama yake na Isa aliambiwa na malaika atazaaa mtoto bila mume, (Hapo ni malaika wengi) Lakini kwenye quran 19:16-22 Imeeleza tena kuwa Jibril akaenda peke yake kumwambia Mariamu atampa mtoto, iweje kule azae kwa uwezo wa Mungu, na huku apewe mtoto na Jibril? kama zile habari za Quran 3:45 kama zingekuwa ni Habari za sahihi, Mariamu asinge muuliza hivi Jibril
قَالَتْ أَنَّى يَكُونُ لِي غُلَامٌ وَلَمْ يَمْسَسْنِي بَشَرٌ وَلَمْ أَكُ بَغِيًّا
Quran 19:20. Akasema: Ninawezaje kupata mtoto hali hajanigusa mwanamume yeyote wala mimi si asherati.

Wakati Kabla ya kwenda Jibril, tayari kuna Malaika walishatangulia kumwambia hivi Mariamu
إِذْ قَالَتِ الْمَلَآئِكَةُ يَا مَرْيَمُ إِنَّ اللّهَ يُبَشِّرُكِ بِكَلِمَةٍ مِّنْهُ اسْمُهُ الْمَسِيحُ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ وَجِيهًا فِي الدُّنْيَا وَالآخِرَةِ وَمِنَ الْمُقَرَّبِينَ
45. (Kumbukeni) Malaika waliposema: Ewe Mariam! Hakika Mwenyeezi Mungu anakupa khabari njema za neno litokalo kwake, jina lake ni Masihi Isa Mwana wa Mariam, mwenye heshima ulimwenguni na Akhera, na ni miongoni mwa wenye kukurubishwa (mbele ya Mwenyeezi Mungu).

Pia isitoshe, mama yake na Issa, yeye hakuwa na mchumba kama alivyo kuwa kwa mama yake na Yesu, yeye alikuwa ameposwa na Yusufu,
Luka 2:4 Yusufu naye aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa mbari na jamaa ya Daudi;
5 ili aandikwe pamoja na Mariamu mkewe, ambaye amemposa, naye ana mimba.

Ndiyo maana alipozaliwa Yesu, watu wengi wakadhani kwamba ni mtoto wa Yusufu
Luka 23: 23 Na Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikuwa amepata umri wake kama miaka thelathini, akidhaniwa kuwa ni mwana wa Yusufu, wa Eli,
Kwa sababu Mariamu, alikuwa ameposwa na Mwanaume kihalali, Lakini maama yake Issa yeye kwa kuwa hakuwa na mchumba, alipochukua mimba siku hiyo hiyo NA Kuzaa siku hiyo hiyo, ndugu zake walishangaaa na kusema,
Quran 19:27. Kisha akampeleka kwa jamaa zake akimbeba. Wakasema: Ewe Maryam! hakika umeleta kitu cha ajabu.
28. Ewe dada ya Harun! baba yako hakuwa mtu mbaya wala mama yako hakuwa asherati.
Tena hapo tunaona kuwa Issa ameitwa kitu cha ajabu, (kwa sababu ni mtoto aliepatkana siku moja) kuna mkanganyiko mwingine mkubwa hapo, mkubwa kuhusu Mariamu, maana ndugu zake wanasema huyo Mariamu ni dada yake na Haruni, na Kibiblia, Da wa Haruni, aliitwa Miriamu, hawa walikuwa ndugu watatu,
Haruni
Musa
Miriamu

Hesabu 26: 59 Na jina la mke wa Amramu aliitwa Yokebedi, binti wa Lawi, ambaye alizaliwa kwake Lawi huko Misri; na huyo Yokebedi akamzalia Amramu Haruni, na Musa, na Miriamu umbu lao.
Sasa Muhammad anakuja kutuchanganyia Habari Miriamu dada yake Haruni, na kumuita Issa,
Pia uongo mwingine wa Jibril kwa Mariamu upo hapa,
26. Basi ule na unywe na uburudishe macho, na kama ukimwona mtu yeyote useme; Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwingi wa rehema ya kufunga swaumu, kwa hiyo leo sitasema na mtu.
Eti kama Mariamu ataulizwa na watu kuhusu Issa, kwa kuwa hatokuwa na majibu, aseme kuwa, leo nimefunga, sitosema na mtu, Sasa hapo hajasema na mtu? “Leo nimeweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kufunga leo sisemi na mtu” Hapo hujasema?
kwa Hivyo Issa Kalenga, Yesu siyo Issa, kwani Yesu yeye kuzaliwa kwake siku zilitimia,
Luka 2: 6 Ikawa, katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia,
7 akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng'ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.

Kwa hivyo huwezi kumringanisha Issa alie zaliwa siku moja, na Yesu ambae siku zake za kuzaliwa zilitimia, sasa Kalenga nami nakuuliza wali moja tu, ukinjibu, basi nitakubaliana nawe kuwa Isa ndiye Yesu, nikatoa Kitabu cha
Mathayo 14:23 Naye alipokwisha kuwaaga makutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake.
24 Na kile chombo kimekwisha kufika katikati ya bahari, kinataabika sana na mawimbi; maana upepo ulikuwa wa mbisho.
25 Hata wakati wa zamu ya nne ya usiku Yesu akawaendea, akienda kwa miguu juu ya bahari.
26 Wanafunzi walipomwona akienda juu ya bahari, wakafadhaika, wakisema, Ni kivuli; wakapiga yowe kwa hofu.
27 Mara Yesu alinena, akawaambia, Jipeni moyo ni mimi; msiogope.

Nikamwambia Kalenga, hapa kwa mujibu wa andiko hili, Yesu alitembea juu ya bahari, sasa Ili Yesu awe ndiye Issa, ni andiko gani ndani ya Quran Issa katembea juu ya bahari? Kama bahari itakuwa kubwa, basi hata kwenye maji ya ziwa, kama ziwa kubwa, basi hata maji ya mto tumuone akitembea juu yake na kama maji ya mto makubwa, basi hata maji ya beseni tu kuna andiko kama hilo la Issa kutembea juu ya maji ndani ya quran?”
Kalenga akajibu kuwa, “Ndani ya Quran hakuna aya inayosema kuwa Issa ametembea kwenye maji” Basi hapo waislamu wakawa kimya, nikamrudishia Mic Ernest aendelee na mkutano maana kazi yangu nimeshaimaliza, kwa kweli Mkutano uliwabariki watu wengi sana, Baada ya siku hiyo Kina Kalenga hawakuonekana tena kuja kwenye mkutano, tukaja kuambiwa, wamerudi Mwanza, basi baada ya kuona Hivyo, ikambidi Sheikh Ramadhani Mazige, wa pale Nansio ambae alikuwa anasifika kwa kuwatupia watu majini, kuhitihisha kikao na kuandaa kisomo cha Albadri (Nitakuja kuwalezea kisomo hicho kikoje na inatumika nguvu gani kumdhuru mtu) Wakasoma Albadiri, Ili Ernest, Abubakari, na Mjuni, wafe lakini wapi, hakuna aliekufa, walipoona hivyo, Sheikh Ramadhani, akaamua kwenda kwa OCD wa kituo cha POLISI, Nansio, akampa hela, ili aje kufunga mkutano wetu, zilipobaki ziku 9 Mkutano uishe, Ernest akaondoka kurudi MWANZA, kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu yeye na familia yake, maana yeye alikuwa ameoa, mimi na Mjuni, ndo ambo hatukuwa na wake, Basi baada ya kuondoka Ernest tukabaki mimi na Mjuni, Tukasema hapa ni kuwapa Gombo Waislamu, Siku ya pili ya sikuu ya Christmas, tukawa uwanjani kama kawaida, tunapiga zetu Gombo, Uwanja umejaa Wakristo pamoja na waislamu, Mezani akawa amekaa Jeshi Kilosa,, Mchungaji Michael Abel, Filipo, me nikaambiwa niende kule kwenye meza ya msomaji, nikasome Surat Yassin kwa Kiarabu, wakati nasoma, Nikaona gari la Polisi linakuja kwa Kasi kubwa, nikajua linaenda kuwashika wauza Gongo pale mtaa wa Mviringo, Kumbe linakuja kwetu, nastukia hilo hapo mbele yangu, Askari wameshashuka kwa haraka, wakanikamata, nikabaki nikaduwaa, Mara Mjuni, Mchungaji, Michael, na Mchungaji Mwingine wa Baptist, ambae aliwaunganisha kina Ernest na Mchungaji Michael Abel, Nikawoana wakipandishwa kwenye Defender, Nami nikaambiwa nipande, nikawa nagoma nikapigwa mtama, ikabidi niingie, kitendo kile kiliwachukiza Wakisto, wakaokota mawe na uanza kulirushia gari la Polisi mawe, nikasikia askari anamwambia mwenzie, Fyatua risasi hewani, Nikasikia PAAAA, nikasema, “Mungu wangu, akifa mtu hapa, si ndo naenda kuozea jela mie?” Ulio wa risasi ukawafanya watu kutawanyika, wakati gari linataka kuondoka, Wafu wakarudi tena wakiwa na kasi ya Mawe, ile gari ya polisi ambayo tumepakiwa, ilipigwa mawe sijawahi kuona, kuna Askari akambiwa ampige mmoja wapo risasi, wakati anaikoki, Bunduki, alipigwa Jiwe la mgongo, mpaka Bunduki akaiachia, mwenzie akaiokota, na kufyatua Risasi, watu wakawatanyika, gari likaondolewa kwa kasi utadhani limebeba majambazi, speed mpaka kituo cha Polisi, tukashushwa huku tunasukumwa, halafu OCD akasema, “Fungeni bendera nyekundu, mkawazue watu wasifike huku” Tulipoingizwa ndani, tukakalishwa, Yule Askari alie pigwa Jiwe, akaja na Rungu, akaanza kutupiga, akampiga yule mchungaji wa BAPTIST kwenye paji la uso, nikaona damu zinamtoka usoni, Yule askari, Me akainua tena kirungu akasema, “Washenzi wakubwa ninyi (akatukana tusi la nguoni) Nimepigwa jiwe kwa sababu yenu, nikamwangalia usoni alikuwa na bonge la sijida usoni, kile kirungu akakishusha ili ampige mchungaji, Mchungaji akarudi nyuma, Kile Kirungu kikatua kwenye goti langu, nikasikia kama mguu umevunjika, nikashindwa hata kutoa sauti kutokana na maumivu ambayo niliyasikia, ki ukweli nilipata maumivu makali sana, akainua tena kile Kirungu anipige mguu wa pili….. UTAENDELEA

Comments