KWA NINI NILIAMUA KUACHANA NA UISLAMU NA KUWA MKRISTO? SEHEMU YA MWISHO.

Na Mtumishi wa MUNGU, Abel Suleiman Shiriwa.
Ushuhuda wa ajabu sana unaendelea, na kama kukusoma sehemu zilizotangulia basi Sehemu ya kwanza FUNGUA HAPA Na Sehemu ya pili FUNGUA HAPA Na kwa sehemu ya tatu FUNGUA HAPA.
Kwa sehemu ya 4 FUNGUA HAPA
Na kwa sehemu ya 5 FUNGUA HAPA na sehemu ya 7 ni FUNGUA HAPA
Ilipoishia: Akainua tena kile Kirungu anipige mguu wa pili, Ndipo akatokea askari mmoja anaitwa George, akakishika kile kirungu, na kunikingia mgongo, na kumwambia yule askari aliyetupiga, “Sasa uawapigia nini? Kwani kuna fujo ambayo wamefanya? Au hujui sheria inaruhusu kutumia nguvu kwa watu wa aina gani? Unawapiga kama majambazi wakati hawa ni watu wa dini?” Yule askari akawa ameondoka, tukabaki na yule Askari aliezuia tusiendelee kupigwa, akatuambia, “Mimi ni Mkristo, huyo alokupigeni ni muislamu, ki ukweli sisi Polisi wa Kikristo tumeumia sana kwa tukio hili ambalo mmefanyiwa, kwani waislamu mara nyingi wamefanya mihadhara yao hapa Ukerewe tena zaidi ya mara 4 hawakushikwa, lakini ninyi mkutao wenu wa Kwanza mmefanyiwa hivi, Poleni sana watumishi” akatoka na kutuletea dawa za kutuliza mauimvu, mimi nikazipokea na kuzinywa, baada ya muda nikaona mguu umeanza kupungua maumivu, siku hiyo tukalala ndani, Ila yule mchungaji walie muumiza, wakamtoa kwenda kumtibia, na kisha wakamwachia, tukabaki watu watano, mimi. Mjuni, Jeshi Kilosa, na Filipo, Asubuhi tukapelekwa Mahakamani, Mwendesha mashitaka alikuwa anaitwa Issa, mashitaka yakawa yale yale ambayo niliyaeleza katika ushuhuda uliopita, kesi ambayo waislamu huifungua kwa kusingizia kuwa, Tumesema Mtume Muhammad alikuwa malaya na alikufa kwa Ukimwi, akasema, “Hawa wasipewe dhamana, kwa sababu ya usalama wao” na kweli tukanyimwa dhamana,
Mahakama na Gereza la Ukerewe haviko mbali sana, kwa hivyo tukatoka pale mahakamani, tukaenda magereza kwa mara ya kwanza nikiwa na miaka 18 Nikaingia gerezani, nikiwa na miezi miwili tu baada ya kuachana na uislamu na kuwa Mkristo, kufika gerezani, tukavuliwa nguo kusachiwa, ki ukweli nilioa kama dunia imenitupa, naingia gerezani, nikiwa mdogo kuliko wote, ki ukweli nilikosa raha, nikamwambia Mchungaji, ‘Kama Ukristo wenyewe ndiyo huu wa kuwekwa ndani, nikitoka basi mimi narudi kwenye uislamu, siwezi kuvumilia mateso haya” Mchungaji akaniangalia na kuniambia, ‘Mwanangu Abubakari, Huu ndo Ukristo wenyewe, hapa ujue ndo unatengeza taji lako, hiki kitakuwa ni ukumbusho wako mbele za Mungu, kumbuka ulivyoachana na Uislamu, shetani hajafurahi, kwa hivyo bado anakuwinda kukurejesha kwenye himaya yake ya Mwanzo, kwa hivyo wewe kuwemo humu gerezani, ni Unabii wa maandiko ambayo Yesu aliyasema” akainuka, akaenda kumtafuta Mnyampala akamuomba ampe Biblia kama itakuwepo, akapewa, na kisha akarudi, akaniambia, kwa sababu unajua kusoma, naomba usome Ufunuo 2:10-11 Nikasoma.
Ufunuo 2:10 Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.
11 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.

Akaniambia kuwa, Yesu amesema, tutawekwa gerezani, tutakuwa na dhiki, ila akasema tuwe waaminifu hata kufa, tukiwa waaminifu, basi tutapewa taji ya uzima, Kwa hivyo sisi Wakristo kupata mateso kwa ajili yake ni jambo ambalo tayari limeshaandikwa, akaniambia nisome tena
1 Petro 4: 13 Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe.
14 Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia.
15 Maana mtu wa kwenu asiteswe kama mwuaji, au mwivi, au mtenda mabaya, au kama mtu ajishughulishaye na mambo ya watu wengine.
16 Lakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hilo.

Maandiko haya yakaniongezea imani, na kuona hakika maneno ya Biblia ni maneno ya kweli, kwa sababu, nimeona yametilimika, nikamwambia Mchungaji, “Ahsante sana kwa maneno mazuri haya, Mungu anisameshe sana kwa yale ambayo nimeyaongea, kwa hivyo kuanzia leo sitothubutu kumkana Yesu hata kama kisu kitapita shingoni mwangu” Akacheka, na kuniambia, “Ubarikiwe sana sasa umeanza kukomaa Kiimani” kisha akaniambia tena, “Usione kwamba tumepelekwa mahakamani, ndo tumefungwa, hapana hapa tuko mahabusu, kwa hivyo usiwaze utajibu pale mahakamani, Mungu mwenyewe atatupigania sisi, hebu soma
Mathayo 10:16 Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.
17 Jihadharini na wanadamu; kwa maana watawapeleka mabarazani, na katika masinagogi yao watawapiga;
18 nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa.
19 Lakini hapo watakapowapeleka, msifikiri-fikiri jinsi mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema.
20 Kwa kuwa si ninyi msemao, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu.
21 Na ndugu atamsaliti nduguye ili auawe, na baba atamsaliti mwana, na wana watawainukia wazazi wao, na kuwafisha.
22 Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.

Kupitia mandiko hayo nikajiskia amani kukaa mahabusu, naweza kusema Mungu alitufunika kwa utufu wake, kwani wafungwa na mahabusu asilimia kubwa, walitupenda, tukawa tunashare nao maandiko, ikifika mida ya kulala tukawa tunaimba nyimbo za Kikrsto, hata waislamu nao wakawa wanaimba, nikaona raha sana kuwemo mle, wapendwa wakwa wanakuja kutuona na kutuletea sabuni na mafuta, vitu vingine tukawa tunawagaiwa wafungwa na mahabusu ambao hawana ndugu wa kuja kuwaona, Nilikaa mle Mahabusu kwa muda wa siku 21, Tukaitwa kwenda Mahakani mimi na Mchungaji tukapata dhamana, Mjuni, Filipo, na Jeshi Kilosa wadhamini wao walichelewa, wakarudishwa mahabusu, baada ya siku mbili wakatolewa kwa REMOVE OLDER
Tukaungana nao kumtukuza Mungu, Mjuni akarudi Mwanza mimi nikabaki Ukerewe, sasa baada ya kutoka gerezani, Nikamuomba mama Happy anipe simu yake nimpigie, dada yangu Zena, mtoto wa mama mkubwa, yeye nilikuwa nimeiandika Namba yake, Nikaamua nibadili sauti, ili nijifanye kama namuulizia Aboubakari, ili nijue kama wameshapata taarifa zangu za kukamatwa basi nikapiga, akapokea, nikaongea kwa sauti nzito, “ASSALAAM ALYEKUM” akaitikia,”Wa’aleykum Ssalaam” Nikamwambia, “Naitwa Abdul, nilikuwa namuulizia Aboubakari yupo hapo?” akajibu, “Aboubakari ni mjinga sana, yupo huko Ukerewe, na kina Simba Ulanga, amefungwa” Nikakata simu, Nikasema, “Dah, kumbe wameshaambiwa, nikajipa moyo potelea mbali”

Nikaendelea kuwepo Ukerewe kwa ajili ya kesi, kila ikifika siku ya kesi, Mjuni anakuja Ukerewe na kuhudhuria kesi, na kisha kurejea Mwanza, kesi ile baada ya kuonekana kuwa, tutashinda kutokana na Ushahidi kukosekana, yule Mwendesha mashitaka, Issa, akamshawishi Jeshi Kilosa, akimbie, ili sisi tufungiwe dhamana, turudi ndani, na kweli Jeshi Kilosa akakimbia, yule mdhamini wake akakamatwa, na kuhukimwa kwenda Jela miezi sita, au kulipa faini ya laki mbili, kwa siku hiyo ikakosekana, ikabidi aende gerezani, alikaa kama siku 6 akatolewa baada ya hela kupatikana, lakini sisi hatufungiwa dhamana, Kuna kipindi cha kesi yetu kusikilizwa, Issa, akampigia mjuni simu kuwa, Kesi itakuwa saa nne, na kumbe ni saa 2 Ili tu tuchelewe dhamana yetu izuiwe , siku hiyo tukaenda saa 4 tukawakuta wenzetu wametoka, tukaenda kuripot tukaambiwa turudi mpaka tar ya kesi, tare ilipofika, Hakimu akatuuliza, kwa nini hatufika, tukawamweleza kuwa, “Mjuni alichelewa kutokana na Meli kupata hitilafu, Hakimu akasema, sasa mnataka Mhakama iwafanye nini?” Tukamwambia, Tusamehewe, kwani hatutarejea tena kufanya kosa hilo. Akasema, “Mmesamehewa” Wakati tunaendelea na kesi, Waislamu wakaja kufanya muhadhara, mimi nikawa naenda kuwauliza maswali, namshukuru Mungu, kwa sababu nilikuwa nawashika sana, mpaka ikafikia hatua wakawa wananifukuza kwenye meza ya maswali, wakawa wanakuja kufanya mihadhara, na kuondoka, baadae sisi Kesi yetu ikafutwa baada ya ushahidi kukosekana, Ile siku ambayo kesi imefutwa, Mchungaji Michael Abel, akasema, Tunaenda kuweka Mkutano kama ule ambao ulitufanya tushitakiwe, na kweli Mkutano ukawekwa.
Ujasiri ule ambao nilimuona nao Mchungaji Michael ulinitia moyo sana, nikawambia, Nibatize (Kwani nilikuwa bado sijabatizwa) Nikaenda kubatizwa, akasema, unataka Jina gani, nikawambia, nataka niwe na ujasiri kama Wako katika Kuihubiri Injili, kwa hivyo, niitwe Abel, kwa hivyo badala ya Aboubakari, nikawa naitwa Abel, mpaka Leo, Tukaendelea na mkutano, Ernest akaja, ulipo malizika, wakaniambia niendelee kubaki Ukerewe, wao waende Mwanza, watengeneze mazingira, yakikaa sawa wataniita, nikakaa Ukerewe, Nikapata Marafiki, akiwemo KADUGUDA, aliekuwa anauza sokoni pale Ukerewe, na Mwingine anaitwa Baba Jose, na pia Stephene, Fundi Semala, na wengineo wengi, ambao walini surpot katika mahitaji mbali mbali, kwa hivyo sikujiona mpweke.
Pia nikawa naendelea kujifunza mambo mengi kuhusu Imani ya Kikristo, nikazidi kuimarika, Siku moja mida ya saa 12 Jioni, nilikuwa natoka kwa Kina Mkama, rafiki yangu, ambae alinipenda kwa sababu ya kuwabana waislamu kwenye maswali, njiani, nikakutana na wale vijana wa MARKAZ ALJAZEERA, wakiwa wamevaa kanzu, wakaniambia, “We Mwana kharamu, tulikuwa tunakutafuta siku nyingi sana, tumashukuru Allah leo tumekupata, tutakachokufanya leo, hutokaa usahau maishani mwako” Nikawaambia, ‘Hamuoni kwamba ninyi mmejifananisha na wanawake, maana mmeniijia mkiwa wanne, mimi niko peko yangu, mnataka kunichangia, hivi mlishona wapi wanaume wenye kujiamini wakamchangia mwanaume mmoja?” Wakasema, “Ngoja tukunje kanzu zetu, mwana kharamu wewe usije ukatuchafulia tutakapo kushughulikia” Nikawaambia, kanzu zenu hizo ndefu ambazo mnaringa nazo, hayo ni mavazi ambayo walikuwa wanavaa wanavaa wanawake”
2 Samweli 13: 18 Naye alikuwa amevaa kanzu ndefu; kwa kuwa kwa nguo hizo huvikwa binti za mfalme waliokuwa wanawali. Ndipo mtumishi wake akamleta nje, akafunga mlango nyuma yake.
Nikawaambia, Kanzu za kiume haziko hivyo, Kanzu za kiume aliambiwa Mussa amtengenezee Haruni, akaambiwa aweke na vitu fulani, zilikuwa fupi, sasa ninyi badala ya kufanya utafiti mjue tofauti ya kanzu ya kiume na kike, ninyi mnajivalia tu” Nikastukia, nimepigwa nondo kichwani, damu zikaanza kunitoka, wakakimbia, wakijua nitaanguka nife, lakini namshukuru Mungu sikufa, nilienda kushonwa, nikauguza kidonda na kupona, baada ya kukaa Ukerewe kwa muda wa miezi 6 baada ya kina Ernst kuondoka, nikaona sina mawasiliano nao, nikaamua nirudi Mwanza, pa kufikia itakuwa nyumbani, Stephene, akanipa Nauli, huyo, nikarudi zangu Mwanza, kufika Pale Ghana, Home, nikamkuata sister Ashura, yupo nje, anamenya ndizi, mimi nikawa nasita kuingia ndani, akaja akanifuata na kuniambia, ‘Ingia ndani sasa unaogopa nini wakati hapa ni kwenu?”
Basi nikapitia mlango wa JIKONI, nikaingia ndani, nikawa nimekaa kwenye SOFA, mama akatoka amevaa Niqabu, (Kininja) basi akafunua ile Niqabu, na kusema, “Naomba hela yangu ambayo nilikupa uende Ukerewe” Mimi nikawa namtazama tu bila kumjibu kitu, akaniambia, “Inamaana hunisikii?” Nikanyamza, akaniuliza, “Umeshakula?” Nikamjibu, “Ndiyo” akamwita Hawa, na kumwambia, “Kamlete soda huyu” Nikastuka, nikasema, mbona anaagiza niletewe soda, wanataka kuniwekea sumu ili nife nini?” Nikajipa moyo kutokana na maneno ya Yesu, aliyosema,
Marko 16:17 Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;
18 watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.

Nikasema moyoni acha walete ninywe, maana Mungu atanilinda, basi nikaletewa soda, nikanywa, wakati nakunywa, mama akaingia chumbai kwake, kwenda kuswali, alipotoka, akaniambia, “Msubiri baba yako mje kuongea, maana alikuwa ana hamu sana na wewe” kweli Usiku baba akaja, nikamsilimia, “Assalaam aleykum” Akasema, “Wa’alayka” Nikaguna, akaingia chumbani na kubadili nguo kisha akasema, “Kabla ya kuoga ngoja kwanza niongee na huyu” Akasema, “Njoo ukae hapa” Nikaenda, akaniamba,”Hivi ni kweli Umeritadi?” Nikamjibu ‘Ndiyo”Akasema “Ewe Abuobakar ulikuwa ni mwalimu mzuri sana wa kiislamu, ni kwa sababu gani umeamua kuritadi? Nikawambia, “Kabla sijakujibu, naomba nichukue quran na Biblia, ili nikupe sababu kimaandiko” akasema, “Sawa chukua” Nikaenda kwenye begi nikachukua, nikakaa, kisha nikawambia, Nimeamua kuwa Mkristo, kwa sababu, Yesu anasema yeye ndiye njia kweli na uzima.
Yohana 14:2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.
3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.
4 Nami niendako mwaijua njia.
5 Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia?
6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.

Nikawambia, baba, “Hapo Yesu amesema, yeye ameenda kuandaa Makao mbinguni, ndiyo maana alipokufa, siku ya tatu akafufuka, kisha akapaa kwenda mbinguni, ili akatuandalie hayo, makao, tena akasisitiza kuwa, yeye ndiye Njia kweli na Uzima, mtu haendi mbinguni bila kupitia njia yake, sasa kwa kuwa mimi ni mtu siyo JINI, ndo maana nimeamua kumfuata Yesu, ulitaka niendelee kumfuata Muhammad ambae yeye alipokufa ikawa moja kwa moja, yupo kaburini, mbinguni hajui kunaendelea nini, tena hajui kuwa atafanywa nini yeye na ninyi
Quran 46: 9. Sema: Mimi si kiroja miongoni mwa Mitume. Wala sijui nitakavyo fanywa wala nyinyi. Mimi nafuata niliyo funuliwa tu kwa Wahyi, wala mimi si chochote ila ni mwonyaji mwenye kudhihirisha wazi
Nikamwambia, nina sababu gani mimi ya kuendelea kuwepo kwa mtu huyu ambae hajui atafanywa nini yeye wala hao wenye kumfuata, hivi kweli wewe una safiri kutoka Mwanza kwenda Dar, Unakutana na Dereva anakwambia, panda kwenye gari langu, unamuuliza, unapajua Dar? Anakwambia, sipajui we twende tu hivyo hivyo,, na akatokea Mwingine, nae akasema, panda kwenye gari langu, me Dar napajua, Utapanda gari gari gani? La anaepajua Dar au asiyepajua?
Muhammad ni Dereva ambae hajui aendako, lakini mtazame Yesu, yeye ni dereva ambae anajua alikotoka na pia anakujua huko aendak”
Yohana 8: 12 Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.
13 Basi Mafarisayo wakamwambia, Wewe unajishuhudia mwenyewe; ushuhuda wako si kweli.
14 Yesu akajibu, akawaambia, Mimi ningawa ninajishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu ndio kweli; kwa sababu najua nilikotoka na niendako; lakini ninyi hamjui nilikotoka wala niendako.

Nilipokuwa nayasoma maandiko hayo baba akawa ananiskiliza kwa makini sana, nikazidi kumwambia, sababu nyingine, ni kuwa, Muhammad yeye hana mamlaka yoyote, kama alivyosema hapa
Quran 7: 188. Sema: Sina mamlaka ya kujipa nafuu wala kujiondolea madhara, ila apendavyo Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa ninayajua ya ghaibu ninge jizidishia mema mengi, wala ovu lisinge nigusa. Mimi si chochote ila ni mwonyaji na mbashiri kwa watu wanao amini.
Nikawambia, “Mtu huyo ambae hana uwezo wa kukemea homa, ikamtoka, wala hana uwezo wa kujipa unafuu, nina sababu gani ya kuendelea kumfuata huyo, na kumwacha Yesu ambae yeye kwanza ana mamlaka yote Mbinguni na Duniani?”
Mathayo 28:18 Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
Pili ana malaka juu ya wote wenye mwili.
Yohana 17:1 Maneno hayo aliyasema Yesu; akainua macho yake kuelekea mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe;
2 kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele.

Tatu anayo malaka kwa walio hai na waliokufa
Warumi 14:9 Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii, awamiliki waliokufa na walio hai pia.
Nikawambia, “Nawezaje kumwacha huyu Yesu ambae Dunia na Mbingu, viko chini ya umiliki wake, nawezaje kumwacha Yesu, ambae watu wote wenye mwili, wana milikiwa na yeye, na pia hata waliokufa nao pia wako chini ya umiliki wake, yaani hata MuhaMmad nae amekufa yupo chini ya mamlaka ya Yesu, sasa nawezaje kumwacha huyu Yesu na kuendelea kuwa chini ya Muhammad ambae hana mamalaka yoyote?” (Hapo nilikuwa natumia Quran Tafsiri ya Sheikh Abdulla Saleh Farsy (ambayo haijawekwa kwenye mtandao) nikazidi kumwambia kuwa, “Isitoshe Muhammad ni mmoja wa watu ambao watapanga foleni siku ya hukumu kusubiri kuhukumiwa
Quran 10: 102. Basi, je! Wanangojea jingine ila (kuwajia) mfano wa siku za (adhabu zilizowafika) watu walio pita kabla yao? Sema, “Ngojeni! Mimi (pia) ni pamoja nanyi katika wanao ngoja.
Huyu yeye yupo kwenye foleni ya kusubiri siku za adhabu, na katika ufafanuzi wa Sheikh Abdulla Farsy amesema.
2:102 Ukimuona mwenzio amenyolewa kwa jambo hilo unalolifanya basi kitie maji upesi kichwa chako, kwani na wewe utanyolewa kama alivyonyolewa.
Nikamwambia, ndiyo maana Waislamu kila siku mnaweka maji kichwani mnapoenda kuswali kwa sababu, mpo kwenye foleni, pamoja na Muhamamd, ila mimi nimemfuata Yesu ambae ndiye hakimu, atakae muhukumu Muhammad na watu wote,
Yohana 5:26 Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake.
27 Naye akampa amri ya kufanya hukumu kwa sababu ni Mwana wa Adamu.
28 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake.
29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.

Sasa hapo angalia mwenyewe Yesu, Hakimu, Muhammad, mtuhumiwa, anasubiri kuhukumiwa, sasa wewe baba unaweza kukaa nyuma ya nani? Mshitakiwa Muhammad au Hakimu Yesu? Tena baba Yesu amesema kuwa, yeye ndiye atakae wafufua watu wote siku ya mwisho, sasa Muhammad kafa, na watu ambao watafufuliwa kwanza ni wale ambao wamekufa katika Kristo Yesu.
1 Wathesalonike 4:16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.
Ufufuo huo wa Kwanza, utawahusu wale tu ambao wamekufa katika Kristo, Muhamamd yeye hakufa katika Kristo, sasa Kama Yesu atagoma kumfufua Muhammad, unategemea mimi nitakuwa mgeni wa nani kama nitaweka tumaini langu kwake? Mimi nimekimbia huko nipo kwa hakimu Yesu” Baba akaniamba “Pamoja na hayo, kumbuka Mwenyezi Mungu amesema kuwa, dini Isiyokuwa ya kiislamu haikubaliwi, na mtu huyo Akhera atakuwa ni mwenye khasara kubwa, kabisa, hebu soma Quran 3:85” Nikaisoma, inasema:
Quran 3: Na anaye taka dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye khasara (kubwa kabisa)
Akasema, ‘Mwanangu huoni kuwa utakuwa ni mwenye khasara kubwa sana Akhera kwa sababu ya kuikataa Dini ya Kiislamu?” Nikawambia “Baba nani amekuambia kuwa mimi nataka niende Akhera kupata faida?” hivi unapajua Akhera?” Akasema, “Hebu niambie ni wapi?” Nikawambia naam, “Akhera ambako wewe umeona kuna kuna faida kwako ukiufuata Uislamu, ni makao yenu ambayo mtakaa milele
Quran 6:98. Na Yeye ndiye aliye kuumbeni katika nafsi moja na nafsi moja. Pako kwa (ajili yenu) mahali pa kukaa milele (napo ni Akhera) na mahali pa kuwekwa muda muda mdogo (npo ni duniani) Hakika tumezichambua Ishara hizi kwa watu wanao fahamu.
Nikawambia, Huko Akhera ambako ninyi mtaenda kukaa milele, ndiko ambako Jehanamu ipo, yaani ndo makao makuu ya Jehanamu”
Quran 78:21. Hakika Jahannamu inangoja wabaya
Ufafanuzi wa Sheikh Farsy katika aya hiyo unasema”
78:21, Jahanamu, ni jina la moto maalumu huko Akhera
Kwa hivyo mimi nikiufuata uslamu, faida ambayo nitaipata ni huo moto wa Jahanamu ambao upo huko Akhera mbako ninyi mnaenda kukaa milele, tena kuna adhabu kubwa sana huko, kama alivyosema Allah
Quran 20: 127. Na hivi ndivyo tutakavyo mlipa kila apitaye kiasi, na asiye amini ishara za Mola wake Mlezi. Na hakika adhabu ya Akhera ni kali zaidi, na Iendeleayo sana
Nikamwambia, kwa hivyo, huko kuna adhabu isiyokuwa na kikomo, lakini Allah akaweka angalizo hil.
Quran 39:26. Basi Mwenyezi Mungu akawaonjesha hizaya katika uhai wa duniani. Na bila ya shaka adhabu ya Akhera ni kubwa zaidi; laiti wangeli jua.
Kwamba, huko khera ambako ninyi mnakwenda, kuna adhabu kali zaidi, laiti mngelijua, basi mngejiepusha na uendaji wa Akhera, maana kasema, laiti wangaelijua, sasa mimi nimejua kuwa, nikiendelea kubaki kwenye uislamu, nikaenda huko Akhera, faida ambayo mimi nitaipata ni hiyo adhabu kali zaidi ya kuuungua na moto, kwa kuwa amesema laiti wangelijua, mimi nimejua kuwa huko hakufai, ndiyo maana nimekimbilia kwa Yesu ambako hakuna hukumu ya Adhabu kwa wale ambao wapo kwa Kristo.
Warumi 8:1 Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
2 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.

Kwa hivyo baba mimi nimepukana na hiyo adhabu ya Akhera, ambayo nanyi kama mngeijua basi mngekimbia kama mimi, kwa hivyo elewa kuwa, mimi sitaki kwenda Akhera (Makao makuu ya Jahanamu), bali nataka kwenda mbinguni, aliko Kristo Yesu
Wafilipi 3:20 Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo;
21 atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake.

Sasa wewe endelea kumfuata Muhammad, ili ufe kama alivyokufa yeye
Quran 52:31. Sema: ngojeni, na mimi pia ni pamoja nanyi katika wanaongojea (Sifi mimi peke yangu nanyi mtakufa vile vile).
Acha Mwanao nibaki na Yesu wangu ambae hata kama nitazikwa leo, basi nitaendelea kuishi
Yohana 11:25 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;
Kwa hivyo tambua kuwa, Muhammad kama alivyokufa, na mpaka leo hana habari yoyote, nawe pia ukifa utakuwa kama yeye, ila mimi nikifa leo, nitaendelea kuishi kama ilivyo ahadi ya Yesu” Nikamtazama baba nikamuona jasho linamtoka, akainuka pale, na kuja kuninyang’anya QURAN, kisha akasema…….. Fuatana nami kwenye mwendelezo wa Ushuhuda kupitia kitabu ambacho nakitaraji kukiandika hivi karibuni, ili ujue hatima yangu na baba ilikuwaje, ujue mpaka leo nimesimama imara, nimepita mapito gani, pia usiache kuniombea ili niweze kufanikisha zoezi hilo la uandishi wa kitabu.

Comments