KWA NINI NILIAMUA KUACHANA NA UISLAMU NA KUWA MKRISTO?” SEHEMU YA 12

Na Abel Suleiman Shiriwa
Ushuhuda wa ajabu sana unaendelea, na kama kukusoma sehemu zilizotangulia basi Sehemu ya kwanza FUNGUA HAPA Na Sehemu ya pili FUNGUA HAPA Na kwa sehemu ya tatu FUNGUA HAPA.
Kwa sehemu ya 4 FUNGUA HAPA
Na kwa sehemu ya 5 FUNGUA HAPA na sehemu ya 7 ni FUNGUA HAPA
ILIPOISHIA
Tulivyoingia ndani, nikamkuta Ustadhi, BASHRI, ambae alinifundisha Thaqaafa, amekaa anaongea na mama, yule mpendwa akasalimia, bada ya Kusema, Assalaam Aleykum, yeye akasema, “Salama leko” moyo ukalipuka, Paaaa, Salama leko tena? Mama Mama na Ustadhi hawakuitikia, wakamtazama kwa mshangao, Nikasema, kimeshasanuka, wakianza kumuuliza maswali kuhusu Uislamu, Mkristo huyu atajibu nini huu si ndo mwanzo wa kuumbuka? Mama akauliza, “Salama leko ni salamu gani katika uislamu?” mimi nikawahi kusema, ‘Unajua mama, huyu mtu amesilimu hana muda mrefu sana, kwa hivyo bado lahaja yake katika Lugha ya kiarabu haijawa sawa, kwa hivyo bado anajifunza kiarabu, ndo maana badala ya kusema,Assalaam aleykum, yeye kasema Salama leko” mama akasema, “Ndo maana kwani nimeshangaa sana, muislamu gani asalimie hivyo? Haya, niambie kijana umesema mnataka kwenda Ukerewe, ni sehemu gani hiyo ambayo ninyi mtafikia?”
Hapa napo nikaona pataleta shida maana mtu mwenyewe niliemchukua ajifanye muislamu, ili nipate ruhusa ya kwenda Ukerewe, hapajui, Nikadakiza tena, kwa kusema, “Aliniambia pale kwenye Msikiti wa Waarabu, natumai itakuwa ni Nansio” yule jamaa akasema, “Ni kweli” mama akasema, “Mimi nashukuru kwa sababu nimekufahamu, maana nilishindwa kumpa ruhusa bila kumjua, yule ambae ataongozana nae, kwa hivyo nimemruhusu, kikubwa tu usalama wake” Nikamshukuru mama kwa kunipa kibali cha kwenda Ukerewe, basi tukapikiwa SATO na ugali, tukala, baada ya kumaliza kula, nikaoga nikachukua begi dogo nikaweka nguo zangu, kisha nikamuaga mama, akanipa Elfu kumi (10000) Tukatoka zetu nje, tukampitia Hassan, tukatembea kwa miguu, mpaka Shule ya Msingi Mwenge, nikamwambia yule jamaa usije ukatembelea maeneo ya pale home, wakakuona, ikawa noma, kwa hivyo siku ambayo mimi nitarudi, tutawasiliana, akasema,”Sawa, nawatakieni safari njema” akaondoka kuelekea Kirumba,
Sisi hao tukapanda zetu gari, mpaka CUSTOM, tukasubiri Meli, hao tukazama zetu kwenda Ukerewe, hapo hatuna simu, Tukafika Nansio, Tukashuka, Nikamuliza Hassan “Sasa tutawapataje kina Ernest na Mjuni, ukizingatia kuwa, sisi hapa hatuna simu?” akasema, “Waliniambia tukifika hapa, tuulizie Kanisa la E.A.G.T watakuwepo hapo” Ikabidi tuanze kuuliza watu, kuna ambao walituelekeza, kwenda pale, hatukuwakuta kina Ernest; Tukazidi kuuliza, mpaka tukafika Mtaa wa Mviringo, hapo tena tukaendelea kuulizia, tukaonyeshwa kanisa, baada ya kuonyeshwa kanisa lilipo, la Mchungaji Michael Abel, tukafika pale, tukawakuta watu wanatoka ndani ya jengo la Kanisa, tukawasalimia, kisha Hassan akawauliza, “Tunamtafuta Mchungaji Michael Abel, tumeelekezwa tuje hapa, tunaweza kumpata?” Mama mmoja akatuuliza, “Kwani ninyi ni kina nani na mnatokea wapi” Hassan, akajibu, “Mimi hapa naitwa Hassan Issa Kalenga, na huyu hapa ni Aboubakari, tunatoka Mwanza, tumekuja huku, kwa ajili ya kuungana na kina Ernest ambao wamekuja huku kwa ajili ya kufanya mkutano wa Injili”
Yule mama akasema, “Karibuni sana kumbe ninyi ndo wale wageni wetu, ambao tuliambiwa na Ernest kuwa, mtakuja, karibuni sana, mimi naitwa Mama Happy, ni shemasi, Ernest, Mjuni pamoja na Mchungaji, wametangulia kwenda nyumbani kwangu, Akawaita na wengine akatutambulisha kwao, wakafurahi sana wakatupokea mabegi yetu, tukaanza kutembea kueleka nyumbani kwa mama happy, njiani tuliongea mengi sana, KUFIKA NYUMBANI kwa Mama Happy tukawakuta Mjuni na Ernest, wanapata Supu ya Samaki, Mjuni akasema, “Karibuni vijana wangu, hiki ni kisiwa cha samaki, mtakula samaki mpaka ziote tumboni” Tukacheka, tukapewa viti tukakaa, na kuanza kuongea, baadae tukapelekewa maji bafuni, tukaoga, nasi pia tukaletewa supu ya Samaki, tukaendelea kuongea mengi, na kukumbushiana mambo yaliyo pita kabla sijawa Mkristo, na muda wa kula chakula ukafika, tukala zetu, kwa mara ya kwanza nikala Ugali wa Muhogo, bila kuchanganywa na Mahindi, usiku kabla ya kulala, wakasema, tufanyeni maombi, nikawa naijiuliza maombi gani? Wakaanza kuimba nyimbo za taratibu, baadae wakaanza kuomba, nikatamani waendelee kuimba, maana zile nyimbo niliona zinanigusa, nikaanza kuona utofauti baina ya ibada ambazo nilikuwa nazifanya wakati ningali bado muislamu, Maombi yale ambayo waliomba, huku tukiwa tumeshikana mikono, niliskia kama kuna nguvu fulani hivi inanivuta, nikaanza kuhisi kama kizunguzungu, ila sikuanguka, baadae nikaja kustuka, nikajihisi mwepesi, nikajawa na furaha, nikasema, “Hakika leo nimefurahi sana kwa kuweza kushiriki Ibada hii maana nilishazoea zangu Msiktini, kwenye Ibada ya kukariri.
Tukaenda kulala, asubuhi ya siku hiyo nilipoamka, Nikachukua mswaki, nikasukutua, kisha nikamfuata Ernest kumsabahi, nikamkuta anajisomea vitabu, akaniambia ‘Abubakari kijana wangu, sasa hivi Mwili wako siyo kitanda cha shetani tena, bali ni Hekalu la ROHO MTAKATIFU, nikamuuliza, ‘Una maana gani kusema hivyo?” akaniambia, “Hujui kwamba ulipokuwa kwenye uislamu, Pua zako zilikuwa ni kitanda cha shetani? Nikamwambia “Me sijui” akasema, sogea hapa, akanipa Kitabu Cha Sahih Bukhari, akanifungulia, kisha akanimbia soma, hapa, basi nami nikasoma.
Amesimulia Abu Huraira (r.a) Mtume (s.a.w) alisema “Mmoja wenu anapoamka kutoka usingizini, basa atawadhe na apandishe maji puani, na apenge mara tatu, kwa sababu shetani alilala ndani ya tundu za pua yake” (Bukhari, Hadithi na. 516, juzuu ya 4)
Niliposoma hapo, ki ukweli mimi mwenyewe nilicheka sana, nikaaanza kusema, “Duh kumbe nilikuwa gizani jamani, yaani kumbe miaka yote hiyo pua zangu zimetumika kama kitanda cha shetani”, Akacheka sana Ernest, akanimbia, ‘Sasa hivi uko Huru, Soma 1 Korintho 3:16
16 Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.

Ernest akaniambia sasa katika mwili wako, anakaa roho mtakatifu, kwa hivyo pua zako kwa sasa zipo salama kwa sababu ni ROHO MTAKATIFU, ndiye akaae ndani yako, nikamwambia, “Unajua Ernest, nilipokuwa kwenye uislamu, mengi sikuwa nayajua, pia, hata vitabu vingi sisi Waislamu hatukuwa tunapenda kuvisoma, yaani rahisi sana kumkuta muislamu akiwa na Biblia kwenye mfuko wa Kanzu, kuliko kuwa na vitabu kama hivi ambavyo vimetafsirwa kwa lugha ya Kiswahili” akasema, Maadam umekubali kuja huku, basi utayajua mengi, akaniambia, mfano mzuri ni kwamba, Biblia imetutaka sisi Wakristo tuwalee watoto katika njia nzuri, ambayo hawataiacha hata wakiwa wazee,
Mithali 22: 6 Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.
Na hata Yesu alipokuja aliwataka watoto wadogo waje kwake, maana ufalme wa Mungu ni watu kama wao,
Luka 18:16 Bali Yesu akawaita waje kwake, akasema, Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa kuwa watu kama hao ufalme wa Mungu ni wao.
Lakini ni tofauti na uislamu, Muhammad yeye alipomuona mtoto mdogo wa mika sita, badala ya kumlea yeye akamtamani, na kuamua kumuoa, kama Mtoto mwenyewe anavyo hadithia hapa
Hadithi ya Aisha (r.a) amesema, Mtume (s.a.w) amenioa nikiwa binti wa miaka sita, tukaja Madina tukafikia kwa Ban Al-Harith Khazraji nikapatwa na homa kali sana mpaka nywele zangu zikakatika katika baadae zikaja kuwa nyingi, Akanijia mama yangu Ummu Ruuman, akanikuta niko katika pembeya nikiwa na rafiki zangu, akaniita kwa sauti ya ukali, nikamwendea hata nisijue anachoniitia akanishika mkono mpaka akanifikisha mlangoni huku nina hema mpaka zilipotulia pumzi zangu akachukua maji akaanza kunifuta kwa maji hayo uso wangu na kichwa changu kisha akaniingiza ndani nikawakuta wanawake wa kiansari mle ndani wakasema, “uwe juu ya kheri na Baraka na uwe juu ya ndege bora, akanikabidhi kwao wakaniweka vizuri, sikustuka isipokuwa alipofika Mtume (s.a.w) asubuhi mama yangu akanikabidhi kwake, nami siku hiyo nilikuwa ni mschana wa miaka tisa” (BUKHARI, HADITHI NA. 234, Juzuu ya 5)
Sasa kama mtume kama huyu anastahili kuatwa? Nikamwambia, “Hapana, kwa kweli, mambo mengi tunafichwa sana, yaani siyo rahisi Sheikh Kufundisha mambo kama kuwa Muhammad alioa mtoto wa mika sita” Enest akaniambia, ndo hivyo mdogo angu, Aisha kwa hofu akanyonyoka nywele, mtoto mdogo anachezea na watoto wenzie,maana yeye akiwa na mika hiyo sita, anaendwa kuozeshwa na mzee wa mika 54, Kina Umar, wakija nyumbani, wanmuta Aisha, eti shemeji,kuonesha kuwa huyu hafai kufuatwa, Hebu tazama haya mafundisho yake,
Kaema Mtume (s.a.w)“Hakika Mwanamme akimtazama Mkewe (Kwa ajili ya matamanio ya kuingiliana) Nae mke akamtazama mumewe (Kwa ajili hiyo) Basi anawatazama Mwenyezi Mungu utazamaji wa rehema, (MUME) akimshika mkewe mkono wake (kwenda kutimiza haja yao) Basi Yanadondoka (Yanatoka) madhambi yao kwenye vidole vyao” (Mkweli Mwaminifu, Juzuu ya 1-2, Hadithi Na. 468, Uk. 206)
Hebu fikiria mdogo wangu Aboubakari, Kweli, mtu umetoka kuua, umetoka kuiba, umetoka kuzini, umetoka kusengenya, unaenda kwa mkeo, unamtazama kwa matamainio ya kumuingilia, mkeo nae akikutazma kwa jinsi hiyo hiyo, mkaenda kufanya mapenzi basi madhambi yenu yanadondoka kupitia Ncha za vidole vyenu, hivi kweli tendo la ndoa linaondoa dhambi? Nikamwambia, ‘Hapo sasa naanza kukupata, ndo nimeweza kuelewa kuwa ni kwa sababu gani Waislamu wengi hukimbilia kuoa sana na nimegundua ni sababu gani qura'n imewataka waislamu kuoa wanawake wanne, wanaoa wake wanne, Ili kama amefanya dhambi, akienda kwa mwanamke huyu na kumkuta yupo katika siku zake, basi anaenda kwa mwingine, ili tu afanye mapenzi, aweze kusamehewa dhambi, ki ukweli haya siyo mafundisho ya Mungu wa kweli, mwezi wa Ramadhani, napo Waislamu hukimbilia kuoa kwa wale mbao wanaishi na wanawake ambao si wake zao, kwani anajua, mwezi huo ni wa toba, ruhusa iliyopo ni ya kumuingilia mkewe halali kwa mujibu wa uislamu, kwa kuwa anajua akishaoa, hata kama atatenda dhambi, akienda kumtazama tu mkewe usiku wa saumu akamuingilia, basi tayari madhambi yake hayo, yanaondoka”
Akiambia, soma tena na Hadithi hiii
Kasema Mtume (S.a.w) “Ogeni siku ya Ijumaa, kwani anaeoga siku ya Ijumaa Basi inakuwa ni kafara kwake, (Yanafurwa madhambi yake baina ya Ijumaa mpaka Ijumaa, na nyongeza siku tatu” (Mkweli Mwaminifu, Juzuu ya 1-2, Hadithi Na. 66, Uk 41)
Nikamwambia, “ tulishafundishwa, na mimi nilikuwa naamini kuwa, kuoga siku ya Ijumaa kunaondoa madhambi ya siku 10 yaani kanza unafutiwa madhambi ya siku 7 Ijumaa-Ijumaa na nyongeza ya siku 3, maana yake hapo tayari ni siku 10, kwa hivyo mtu unaweza kufanya maovu yako, ikifika siku ya Ijumaa unaenda kuoga, tayari msamha unaupata,” akaniambia, hayo ni mafundisho ya Nabii wa uongo, maana Mungu wa kweli anasema hivi,
Yeremia 2: 22 Maana ujapojiosha kwa magadi, na kujipatia sabuni nyingi, lakini uovu wako umeandikwa mbele zangu, asema Bwana MUNGU.
Kwa hivyo hata kama utaoga Ijumaa 100 tambua kuwa uovu wako bado umeandikwa mbele za Mungu, salama ya mtu ni kuja kwa Yesu, na kutubu dhambi zake, na kushikamana maagizo ya Mungu,
Tuliongea mengi sana, Nikaanza kuona kuwa, kwa Yesu sijapoteza kitu kabisa,Mchana kina Ernest Wakaenda kufuatilia kibali cha Mkutano, wakawa wamekipata, Kesho yake tukaanza mkutano wa Injili, tukivihusisha Vitabu vyote, Biblia pamoja na Quran na Vitabu vya Hadithi, Siku ya Kwanza muitiko wa watu haukuwa mkubwa sana, Ile Siku ya 3 Watu wakawa wameongezeka, Siku hiyo nikaambiwa, nisome Quran kwa kiarabu, na kisha nifasiri, nikafanya Hivyo, Wakristo wakafurahi sana, Waislamu wakashangaa sana, wakawa wanaijuliza hawa Wakristo wamezaje kujua Kiarabu? Bila shaka wamemnunua huyu Kijana wa Kiislamu, kwa kumpa hela, ili aje huku kuudhalilisha uislamu, kwani Wakristo hawajui Kiarabu, kwa hivyo wameona wakiwa wao tu tuwabana kwenye kiarabu, kwa hivyo tukajipange, kesho tujue nini tutafanya, na huyu kijana lazima tumshikishe adabu (hayo nilielezwa na Mkristo ambae alikuwa karibu nao) Siku hiyo tukamaliza,Waislamu baada ya Kunisikia nasoma Kiarabu, wakaenda Kuhimizana kesho waje Kufanya Fujo, Kwa hivyo wale Wanafunzi wa CHUO cha Markaz Aljazeera kilichopo Ukerewe, wakatawanyishwa siku hiyo, Watu wakapata habari, akaja kutuambia, tukasema, hakuna shida, Injili ni lazima Ihubiriwe, Basi muda wa Mkutano ukaanza, somo likapelekwa, Msomaji akiwa Mjuni, Mpeleka Somo ERNEST, mimi nikawa nimekaa kwenye kiti, karibu na Ernest, Nikastukia, Waislamu hao Mezani, Kuangalia, nikagongana macho na HAJI SALUMU, huyu ni Muha wa Kigoma, ila tulisoma wote Madrsa Thaqaafa, Tena Darasa moja, na tulikuwa tunakaa dawati moja, na Nyumbani alikuwa anakuja, na wanamfahamu, aliondoka Thaqaafa kabla me sijaacha, Huku ameshika Jiwe, akaniambia, “Aboubakari kumbe wewe ndo ndo tuliopewa Taarifa zako kuwa, umenunuliwa na Hawa Makafiri uje kuwasomea Quran kwa Kiarabu?” Moyo ukawa kama umekufa GANZI, sikuogopa Jiwe ambalo alikuwa amelishika mkononi, Hofu yangu ikiwa, kwa mama, amenipa Nauli nije Ukerewe kufanya Da’awa (Kuringania Uislamu na kuwavuta Wakristo kwenye uislamu) Leo rafiki yangu Haji, kanikuta hapa nikiwa kwenye Mahubiri ya Kikrsto tukiwataka Waislamu waje kwa Yesu, Akitoka hapa si ataenda kumwambia mama, halafu iwe msala kwangu? Mama si ataniua mie, Nikainuka pale kwenye Meza, nikamtazama HAJI, nikamuona anauinua Mkono wake ambao ulikuwa umeshika Jiwe……. UTAENDELEA
Usikose sehemu ya 13 ya Ushuhuda huu.

Comments