KWA NINI NILIAMUA KUACHANA NA UISLAMU NA KUWA MKRISTO?” SEHEMU YA 10

Na Abel Suleiman Shiriwa, siku ya kufunga ndoa.
Ushuhuda wa ajabu sana unaendelea, na kama kukusoma sehemu zilizotangulia basi Sehemu ya kwanza FUNGUA HAPA Na Sehemu ya pili FUNGUA HAPA Na kwa sehemu ya tatu FUNGUA HAPA.
Kwa sehemu ya 4 FUNGUA HAPA
Na kwa sehemu ya 5 FUNGUA HAPA na sehemu ya 7 ni FUNGUA HAPA
Wakati nawaza kutoka nduki kabla tatu hajanisemesha, Nikamuona anaelekea uani (Chooni) Nikamwambia Mzee, “Endele kuimbisha, me sauti imekataa” Mzee akaimbisha, tukatoka pale, me nikawa sina amani kabisa, tukaendelea kupiga dufu, mpaka saa 9:30 Usiku, tukaondoka zetu kurudi nyumbani, ili tule daku, ki ukweli daku ambayo tulikuwa tunakula siyo rahisi mtu kusikia njaa kali, nyakati za mchana, make mahaage yale yanajaza gesi sana tumboni, UKIFIKA MUDA WA KWENDA KUSWALI swala ya alfajiri, mimi nikawa nakacha, Siendi kusali, wakawa wanashangaa home, mbona siku hizi nimebadilika, kufundisha napo nikawa nimeachana, na miongoni mwa wanafunzi wangu, alikuwepo mwanamke mmoja anaitwa Mama Irene, mumewe alikuwa ni Mkristo, nilimsaidia sana mama Irene kumshawishi mumewe awe muislamu, baada ya kusilimu, mtoto wao nae wakambadilisha jina na kumuita, Husna, Nilipokuwa nakumbuka matukio ambayo nilikuwa nimeyafanya kwa kuwasilimisha Wakristo wakati ule nikiamini kwamba ni imani ya kweli, kumbe nilikuwa nimewapeleka katika shimo la moto wa milele, bila kujua kuwa niliwadanganya, baada ya kuwa mimi nimedanganywa, bila kujua kuwa nimedanganywa,
Nikawa na shauku siku moja niweze kuwarejesha kwenye imani ambayo walikuwepo awali ambayo mimi nimeiendea, basi wakati naendelea na mfungo wa mwezi wa Ramadhani, 10 la mwisho, tukawa tumeenda mjini, mimi mzee pamoja na Juma, ulipofika muda wa swala, basi wakasema twendeni msikitini, nikasema, hapa nisipoenda lazima watanitilia mashaka, nami sikutaka iwe hivyo, basi ikabidi tu niingie kuswali, nilienda kuswali, nikawa kama nafanya tu mazoezi ya kuinama, na kuinuka, bila kusema cho chote, hofu yangu ni kufukuzwa, tuliporudi nyumbani, baada ya kufuturu wakasema, twendeni kwenye swala ya Tarawekhe, me nikasema, ‘Sijisikii vizuri, kwa hivyo wao wakaondoka, me nikabaki pale nyumbani, nikaingia zangu ndani na kuchukua Quran tafsiri ya Kiswahili, na Biblia nikaanza kujisomea, nilikuwa nasoma Surat Ibrahiim, (Sura ya 24) nilipokuja kufika ile aya 22 Nilistuka sana, kuisoma aya hii, nikasema, kumbe tunavyosoma kiarabu tunafichwa mambo mengi sana, hebu ngoja niinukuu
ﻭَﻗَﺎﻝَ ﺍﻟﺸَّﻴْﻄَﺎﻥُ ﻟَﻤَّﺎ ﻗُﻀِﻲَ ﺍﻷَﻣْﺮُ ﺇِﻥَّ ﺍﻟﻠّﻪَ ﻭَﻋَﺪَﻛُﻢْ ﻭَﻋْﺪَ
ﺍﻟْﺤَﻖِّ ﻭَﻭَﻋَﺪﺗُّﻜُﻢْ ﻓَﺄَﺧْﻠَﻔْﺘُﻜُﻢْ ﻭَﻣَﺎ ﻛَﺎﻥَ ﻟِﻲَ ﻋَﻠَﻴْﻜُﻢ ﻣِّﻦ
ﺳُﻠْﻄَﺎﻥٍ ﺇِﻻَّ ﺃَﻥ ﺩَﻋَﻮْﺗُﻜُﻢْ ﻓَﺎﺳْﺘَﺠَﺒْﺘُﻢْ ﻟِﻲ ﻓَﻼَ ﺗَﻠُﻮﻣُﻮﻧِﻲ
ﻭَﻟُﻮﻣُﻮﺍْ ﺃَﻧﻔُﺴَﻜُﻢ ﻣَّﺎ ﺃَﻧَﺎْ ﺑِﻤُﺼْﺮِﺧِﻜُﻢْ ﻭَﻣَﺎ ﺃَﻧﺘُﻢْ ﺑِﻤُﺼْﺮِﺧِﻲَّ
ﺇِﻧِّﻲ ﻛَﻔَﺮْﺕُ ﺑِﻤَﺎ ﺃَﺷْﺮَﻛْﺘُﻤُﻮﻥِ ﻣِﻦ ﻗَﺒْﻞُ ﺇِﻥَّ ﺍﻟﻈَّﺎﻟِﻤِﻴﻦَ ﻟَﻬُﻢْ
ﻋَﺬَﺍﺏٌ ﺃَﻟِﻴﻢٌ

Quran 14:22, Na shetani atasema itakapokatwa
hukumu. Hakika Mwenyeezi Mungu alikuahidini
ahadi ya kweli, nami nilikuahidini, lakini
sikukutimizieni. Wala sikuwa na mamlaka juu
yenu isipokuwa nilikuiteni nanyi mkaniitika. Basi
msinilaumu bali jilaumuni wenyewe, siwezi
kukusaidieni, wala nyinyi hamuwezi kunisaidia.
Hakika mimi nilikataa kunishirikisha kwenu toka
zamani, hakika madhalimu watakuwa na adhabu

yenye kuumiza.
Nikajiuliza kwa mujibu wa andiko hili, hapa kuna ahadi mbili, ahadi ya Mungu, na ahadi ya shetani, ahadi moja ni ya kweli na ahadi nyingine ni ya uongo, ahadi ya Mungu ndiyo yenye kutimia, na ndiyo ahadi ya kwanza kwa wanadamu, ahadi ya pili ni shetani, na ni ahadi ambayo si yenye kutimia, kuna kundi moja la watu hapa ambalo litamwendea shetani, kundi ambalo liilkuwa likimwabdu shetani ambae alkuja kwa sura ya kimungu, na watu wakamwabudu, na akawa ametoa ahadi kwao, ambazo siku ya mwisho, watakapo mwendea atakataa kuwatimizia,kwa sababu hana uwezo huo wa kuzitimiza, ila Mungu ahadi zake ni zenye kutimia, shetani atawakana kwa kuwaambia, yeye aliwaita tu nao hao wakamwitikia, tena anasema, hakuwa na malaka juu yao, kwa hivyo wakati yye anapokea adhabu hizo, hana uwezo wa kuwasaidia, wala wenyewe hawana uwezo wa kumasaidia, kumbukumbu ikanijai wakati ule nafanya harakati za ujenzi wa Miskiti, kuna ustadhi mmoja alibeba jiwe kubwa sana, tukamwambia, “vipi kama likianguka likakuponda?” akasema, hapa nafanya hivi kwa sababu Allah ameahidi kwenda kuniozeshoa wanawake 72 Mahurulaini, kwa hivyo jiwe hili ni kwa ajili ya ahadi hizo, nikasema, hii ni ahadi iliyokuja mika 615 baada ya Kristo, ambayo Muhammad ametoa ahadi kwa waislamu kuwa, siku ya mwisho, watakwenda kuozwa wanawake wenye kupendeza wenye macho makubwa kama mayai ya mbuni.
ﺇِﻟَّﺎ ﻋِﺒَﺎﺩَ ﺍﻟﻠَّﻪِ ﺍﻟْﻤُﺨْﻠَﺼِﻴﻦَ
Quran 37:40. Isipokuwa waja wa Mwenyeezi
Mungu waliosafishwa.
ﺃُﻭْﻟَﺌِﻚَ ﻟَﻬُﻢْ ﺭِﺯْﻕٌ ﻣَّﻌْﻠُﻮﻡٌ
41. Hao ndio watapata riziki maalumu.
ﻓَﻮَﺍﻛِﻪُ ﻭَﻫُﻢ ﻣُّﻜْﺮَﻣُﻮﻥَ
42. Matunda na wao wataheshimiwa.
ﻓِﻲ ﺟَﻨَّﺎﺕِ ﺍﻟﻨَّﻌِﻴﻢِ
43. Katika Bustani zenye neema.
ﻋَﻠَﻰ ﺳُﺮُﺭٍ ﻣُّﺘَﻘَﺎﺑِﻠِﻴﻦَ
44. Juu ya vitanda vya fahari wakikabiliana.
ﻳُﻄَﺎﻑُ ﻋَﻠَﻴْﻬِﻢ ﺑِﻜَﺄْﺱٍ ﻣِﻦ ﻣَّﻌِﻴﻦٍ
45. Wakizungushiwa kikombe chenye (kinywaji)
safi.
ﺑَﻴْﻀَﺎﺀ ﻟَﺬَّﺓٍ ﻟِّﻠﺸَّﺎﺭِﺑِﻴﻦَ
46. Cheupe chenye ladha kwa wanywao.
ﻟَﺎ ﻓِﻴﻬَﺎ ﻏَﻮْﻝٌ ﻭَﻟَﺎ ﻫُﻢْ ﻋَﻨْﻬَﺎ ﻳُﻨﺰَﻓُﻮﻥَ
47. Hakina. madhara, wala hakiwaleweshi.
ﻭَﻋِﻨْﺪَﻫُﻢْ ﻗَﺎﺻِﺮَﺍﺕُ ﺍﻟﻄَّﺮْﻑِ ﻋِﻴﻦٌ
48. Na pamoja nao watakuwa wanawake wenye
macho mazuri matulivu.
ﻛَﺄَﻧَّﻬُﻦَّ ﺑَﻴْﺾٌ ﻣَّﻜْﻨُﻮﻥٌ
49. Hao wanawake kama mayai (ya Mbuni) yaliyohifadhiwa.

Nikaendelea kuzisoma habari hizi kupitia kitabu cha
RAHA ZA PEPONI, KILICHOANDIKWA NA SHEIKH KHAMIS IBRAHIMU
P.O. BOX 2822 Mwanza Tanzania
Mobile +255714 502 620
+255783 326 466
+255766 431 675
Mshauri:
Ustadhi AbdulShakur Maulid/
Katika ule ukurasa wa 52 Sheikh anasema,

ANASEMA MWENYEZI MUNGU (Subuhaanahu
wata’alaa)
”…. Na humo watapata wanawake walio takasika
(Na kila mabaya na machafu)….” (Quran 2;25)
Na kila watakapokuwa wanaingiliwa na waume
zao watakuwa ni mabikira. Bikira hii haishi kwa
kuingiliwa, isipokuwa inakuwa mpya, hatoki
damu wala kusikia maumivu yoyote.
Mtu atapewa nguvu za watu 100 katika unywaji
na uingiliaji; kisha ataongozewa nguvu zingine
zaidi, mme atamwingilia mke wake kama
alivyokuwa akimwingilia hapa Duniani, lakini
peponi ni kwa muda mrefu, ni miaka 80 ya huko
akhera, bila kufika kileleni (Kutokwa shahawa)
Ifahamike siku moja ya akhera ni sawa na mika
1000 ya huku duniani. Kwa hisabu ya huku duniani
ni miaka 28,000,000, Miaka Milioni 28! Wakati
wote huo wanasikia ladha nzuri mno na raha
kubwa ajabu! Hizo ndizo neema za Allah peponi!
Basi, Hakika tutafute Radhi za ALLAH na kila
mara tumuombe ALLAH atujalie tuwe miongoni
mwa watu wema AMIN. (Mwisho wa kunukuu)..

Sheikh Kitabu hiki amekuja kukirudia upya kwa kuweka namba zake, mwanzoni alipoandika hakuweka contact, waislamu walimshauri aweke contact, ndo akaamua kuweka, ila maneno ni yale yale, Nilipokuwa natafakari ahadi hizi, nikawa najiuliza maswali mengi, mwanamke huyo bikira yake ambayo haishi, atakuwa anaingiliwaje? Mtu mmoja atapewa nguvu za wanaume mia, katka kula na pia katika kumuingilia mwanamke, tena isitoshe, Wanawake wako 72, Na mwanamke mmoja anaingiliwa kwa muda wa mika 80 kwa hisabu ya miaka ya akhera, ambayo kwa hapa duniani, ni sawa na miaka milioni 28 Mwanaume bado yupo juu ya kifua cha mwanamke, hao wengine 71 wapo sijui chumbani, wanasubiri mwenzao amalize zamu yake ya kuingiliwa, na wao waingiliwe, sasa kama mwenzao mmoja tu, anaingiliwa kwa miaka hiyo milioni 28, bila mwanaume kumwaga mbegu za uzazi, (Na haijulikani atamwaga lini) sasa hao wanawake wengine watakuja kuingiliwa lini? Huyo wa 72 zamu yake itamfikia lini ikiwa tu mwenziwe wa kwanza anaingiliwa kwa mika milioni 28 bila mzee kufika magogoni? Nikakumbuka pia tulivyokuwa tunafundishwa kuwa, mislamu akiua, (akijitoa muhanga) malipo yake, ni hayo ya wanawake, nikaanza kupata picha kuwa, ndiyo maana waislamu, kuua kwao, sio ajabu, wala wao kufa siyo jambo kubwa, wanatamani kuua na wao wauawe, ili wawahi kwenda huko, kupewa wanawake hao, maana wamea ahidiwa hivi
Quran 9:111. Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo. Wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu - wanauwa na wanauwawa. Hii ni ahadi aliyo jilazimisha kwa Haki katika Taurati na Injili na Qur'ani. Na nani atimizae ahadi kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini kwa biashara yenu mliyo fanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.
Malipo yo baada ya kuua ni haya
ﻣُﺘَّﻜِﺌِﻴﻦَ ﻋَﻠَﻰ ﺳُﺮُﺭٍ ﻣَّﺼْﻔُﻮﻓَﺔٍ ﻭَﺯَﻭَّﺟْﻨَﺎﻫُﻢ ﺑِﺤُﻮﺭٍ ﻋِﻴﻦٍ
Quran 52:20. Wakiegemea juu ya viti vya fahari
vilivyopangwa safu, na tutawaoza wanawake
weupe wenye macho makubwa (ya vikombe)

Nikazidi kuamini kuwa, huku nilikuwa nimepotea, kabisa, pepo gani hiyo ya ngono tu? Ina maana hawa wanawake ambao waislamu wameahidiwa ndiyo sababu kubwa ya waislamu kufanya mauaj? Kama si ahadi hii dunia si aingekuwa sehemu tulivu”, na pia nikawa najiuliza, mbona wanawake wengi wao hawafanyaji mauaji kama wafanyavyo wanaume? Nikakumbuka kuwa Muhammad yeye aliwataka wanawake watoe sadaka kwa wingi kwa sababu wao ndiyo wengi zaidi motoni, pia ni wapungufu wa dini na akili.
Hadithi ya Abuu Said Al Khudryi (r.a) amesema, Mtume (S.a.w)
Alitoka katika Idd ya Adh-ha au ya Fitri kwenda Al-Musalla(Mahali pa kusalia) akapita kwa wanawake, akawaambia, “Enyi wanawake toweni sadaka kwani nimeoneshwa ninyi ndiyo wengi zaidi motoni”
Wakauliza, “Kwa sababu gani EWE Mtume wa Allah?” Akawajibu, “Mnazidisha sana laana na hamuwafanyii wema waume zenu. Sikumuona miongoni mwa wapungufu wa akili na dini kama nyie, Mwanaume mwenye busara anaweza kupotoshwa na mmoja wenu” Wakauliza EWE mtume wa Allah nini upungufu wa dini yetu na akili yetu?” Akasema, “Hivi hamjui kuwa ushaHIDI WA wanawake wawili ni sawa na ushahidi wa mwanaume mmoja?” Wakajibu, “Hilo tunalifahamu” Aksema. “Huo ndio upungufu wa akili. Hivi hamjui mwanamke anapokuwa na Hedhi hasali na hafungi?” Wakajibu, “Hilo tunalifahamu” Akajibu, Huo ndiyo upungufu wa Dini yake” (BUKHARI, HADITHI NA. 301, JUZUU 1)

Nikasema, dah, mama yangu namuona huruma kweli, sijui nimwambie kuwa, hapo alipo siyo salama, ila nikasema, nisije nikaanzisha balaa jingine, Nilipokwa katika kutafakari, waislamu wanaua, ili wakapate wanawake, hivi wanavyoua wana hakika kuwa ni kweli watakwenda kuwapata hao wanawake? Kama ikiwa Allah mwenyewe ambaye amaewaambia waue ili akawapewanawake hao peponi, yeye mwisho wake wake, ni motoni, kama hadithi hii isemavyo
Hadithi ya Anas Ibni Malik (r.a) kuwa Mtume
(s.a.w) amesema jahanamu itaendelea kusema,
“Je, kuna nyongeza”? Mpaka Allah atakapoweka
humo unyayo wake na hapo utasema, Qat Qat
(inatosha inatosha) naapa kwa nguvu zako na
zile sehemu zake nyingine zitakaribiana na kuwa
pamoja” (Bukhari Hadithi Na. 654, Juzuu ya 8)

Nikajisemea, hao wanawake atawapaje wakati yeye mwenyewe mwisho wake ni motoni, nikakumbuka ile aya ya 22 ambayo Shetani, atasema kuwaambia wale ambao watamn’ang’ania, awape ahadi zile ambazo yeye amewaahidi nae atawakana kwa kuwaambia kuwa niliwaahidini sawa, lakini, sina uwezo huo wa kukutimizieni, ninyi hamuwezi kunisaidia, wala mimi siwezi kuwasaidia, nikajua, huyu lazima atakuwa Allah, maana ameahidi kuwapa wanawake, tena kwa kuwaua wakristo,
Nikaona hapa ni kwa namna gani wenzangu wamepotea, nikayakumbuka maandiko ya Yesu aliyosema, baada ya kuendewa na masadukayo ambao nao walitaka kujua, kama kweli kiyama ya wafu ipo basi kutakuwa na kuoa na kuolewa, Yesu alijibu hivi,

Mathayo 22:23 Siku ile Masadukayo, watu wasemao ya kwamba hakuna kiyama, wakamwendea, wakamwuliza,
24 wakisema, Mwalimu, Musa alisema, Mtu akifa, akiwa hana watoto, ndugu yake na amwoe yule mkewe, ili ampatie nduguye mzao.
25 Basi, kwetu kulikuwa na ndugu saba; wa kwanza akaoa, akafariki, na kwa kuwa hana mzao, akamwachia nduguye mke wake.
26 Vivyo hivyo wa pili naye, na wa tatu, hata wote saba.
27 Mwisho wa wote yule mwanamke akafa naye.
28 Basi, katika kiyama, atakuwa mke wa yupi katika wale saba? Maana wote walikuwa naye.
29 Yesu akajibu, akawaambia, Mwapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu.
30 Kwa maana katika kiyama hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika mbinguni.

Nikasema, kweli ndugu zangu waislamu wanapotea kwa sababu hawajui maandiko wala uweza wa Mungu wa kweli, maana kiyama, baada ya ufufuo watu hawataoa, wala kuolewa, ahadi ya kweli ambayo imetangulia kuwepo kabla hata quran haijakuwepo, ina maana kama waislamu wangejua kuwa ahadi hizo ambazo wameahidiwa ni za uongo, na allah mwisho wake ni motoni basi wangeshakimbia huko kama mimi, ila mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao ili isiwazuikie Nuru ya Injili ya Kristo kama ilivyo nizukia mimi.
2 Korintho 4:3 Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea;
4 ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.

Nikawa nashauku kubwa, kwa Mungu awafungue ndugu zangu, angalau na wao iwazukie Nuru ya Injili ya Kristo ili wagundue kuwa allah ambae amewa ahidi kuwa atawapa wanawake, ambao watafanya nao ngono, mwisho wake ni motoni, kwa hivyo hawezi kuwapa, Nikajawa na uchungu mwingi, kuona wenzangu wanavyoamini kuwaua Wakristo wanamtolea Mungu Ibada, wakati sivyo kama alivyosema Yesu
Yohana 16: 1 Maneno hayo nimewaambia, msije mkachukizwa.
2 Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada.
3 Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi.

Nikawa nasema kama waislamu wangemjua Yesu, basi wasingekuwa wanaua ili wapate wanawake peponi bali tu wangempokea Yesu na kuyafanya mapenzi yake, ili awape uzima wa milele, usiku huo niliutumia vema kutafakari mengi, pia nilipokuwa nasoma Kitabu cha Mathayo, sura ya 24, Niliguswa na kitu hapa
Mathayo 24: 29 Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika;
30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi.
31 Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.

Kwanza hapo niliona ni namna gani Yesu alivyo wa muhimu katika maisha ya manadamu, kwani yeye ndiye atake kuja, kuwatuma malaika zake kuwakusanya wateule wake toka mwisho huu wa mbingu, mpaka mwisho huu, inamaana hapo, anakuja kuwachukua wale walio wake, ili waende kuingia katika uzima wa milele, sasa waislamu hapo watakuwa wapi waati wao wanamtumaini Muhammad na kwenda kupata wanawake peponi ahadi ambazo si zenye kutimia? Ina maana kama wangejua basi wote wangekua kaa mimi nilivyo, pia nikawaza hapa Yesu amesema kuwa, Ishara za mwisho wa dunia ni nguvu za mbinguni kutikisika, nikajiuliza mbona Muhammad yeye alifundisha kuwa dalili za kiyama, ni kutingishika kwa matako?
Hadithi ya Abuu Huraira (r.a) Kuwa Mtume )S.a.w) amesema, Hakitasimama Kiyama mpaka matako ya wanawake wa kabila la Dausi yatingishike kulizunguka Dhil-al-Khalaswa.
Dhil-al-Khalaswa, ni sanamu ambalo walikuwa wakiliabudu kabla ya Uislamu” (BUKHARI, HADITHI NA. 232, JUZUU YA 9)

Nikawa najichekea peke yangu, najiuliza, ina maana kwa mujibu wa uislamu, nguvu ya mbinguni ni matako? Maana Yesu kasema kuwa, nguvu za mbinguni zitatikisika, Muhammad yeye anasema, matako ya wanawake ndiyo yatakayotisika, nikasema kweli Ndugu zangu wamo gizani aisee.
Ki ukweli siku hiyo nilikumbuka mengi sana, maandiko ya Biblia ambayo nilikuwa nayasoma, yakaanza kuningia vema, nikaona sijapotea, kabisa kuwa Mkristo, nikaanza kuwaonea wivu wale amabo walikua tayari kuuawa na waislamu kwa ajili ya Kristo, maana roho zao zipo chini ya madhabahu ya Mungu, zikiitazama duniani na hao wauaji wanavyoendelea kuua wakidhani wanamtolea Mungu ibada.

Ufunuo 6: 9 Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao.
10 Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?
11 Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vile vile kama wao.

Nafsi yangu ikajutia sana kwa kitendo kile nilicho kifanya saa 10 Jioni, cha kurejea msikitini kusujudu wakati imani hiyo nilishaikana, Nikasema, kama maandiko yananitaka niwe jasiri, kwa nini niogope kufa?
Ufunuo 20: 4 Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.
Nilipolisoma andiko hili, nikasema, Leo liwalo na liwe, kama ni kufa acha tu nife, nimechoka kuendelea kujificha, maana Ernest aliambia siku ile ya mwanzo kuwa, mtu akimkana Yesu, Yesu nae, atamkana siku ile ya Mwisho, nikasema, tangu nimempokea Yesu, siyafanyi yale ambayo wanayafanya Wakristo, hatimae nimerejea kwenye matendo yale ya Kiislamu, sasa nikifika hapa ghafla nitaenda wapi? Wakati maandiko yanasema, wanaokufa kwa Kristo hao ndiyo wenye kupumzika
Ufunuo 14:13 Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
Nikasema, Yesu nisamehe, kwa vile ambavyo nimekukana, naomba unipe ujasiri na ufungue njia, niweze kutoka hapa, nikakutumikie wewe kwa uhuru, nikajilaza kitandani, usingizi ukanipitia, nakuja kushituka, Mzee ananipiga piga miguu, akaisema, “Abubakari inuka, muda wa kwenda kupiga ngoma za daku umewadia” Nikainuka na kukaa, Nikamambia, “Unasemaje wewe mjinga?” Mzee akasema, “Unaniita me mjinga?” Nikastukia nimepigwa kofi Paaaaa, Niliinuka pale Nikakunja ngumi, nikasema, wewe mpumbavu huwezi kunipga kofi kwa habari zako kijinga hizo, nikapige dufu, kwani umeambiwa me ni Musilamu?”……. UTAENDELEA
Usikose sehemu ya 11 ya ushuhuda huu.

Comments